Upofu

Upofu 가사

원문 언어SW
조회수5
가사 좌표

원문 가사

SW
번역이 아직 없습니다. 원문 가사를 표시합니다.
18
Mi kweli natamani siku iwezekane Nifumbue macho mi kuona Nijue sababu gani, unanipenda sana Wakati siwezi mi kuona? Mi kweli natamani siku iwezekane Nifumbue macho mi kuona Nijue sababu gani, unanipenda sana Wakati siwezi mi kuona? Mara nyingi peke yangu nawaza Namuomba Mungu nisije kukwaza Nikaja kukupa maudhi na nafsi kuichoma Chei, tena usiku mzima nalia darling Napiga goti kwa Mola nasali Azidi tupe baraka tusije kosa dona Eh, mi macho yangu nimejaliwa mboni lakini nuru sina Ningekuwa na uwezo ningefanya kazi nikuhudumie Upofu wangu ndo kikwazo kikubwa, mwenzako raha sina Lakini unanijali, mbali na mengi unanipenda sana Mi kweli natamani siku iwezekane Nifumbue macho mi kuona Nijue sababu gani, unanipenda sana Wakati siwezi mi kuona? Mi kweli natamani siku iwezekane Nifumbue macho mi kuona Nijue sababu gani, unanipenda sana Wakati siwezi mi kuona? Nasikia kuna rangi ya upendo Ili upendwe kuna pozi za mwendo Utanashati, udambudambu na urembo mi sina Mi natamani nitazame Kwa ardhi na mbingu nilalame Nipande mawingu na niiname Uwenda nikaona Eh, mi macho yangu nimejaliwa mboni lakini nuru sina Ningekuwa na uwezo ningefanya kazi nikuhudumie Upofu wangu ndo kikwazo kikubwa, mwenzako raha sina Lakini unanijali, mbali na mengi unanipenda sana Mi kweli natamani siku iwezekane Nifumbue macho mi kuona Nijue sababu gani, unanipenda sana Wakati siwezi mi kuona? Mi kweli natamani siku iwezekane Nifumbue macho mi kuona Nijue sababu gani, unanipenda sana Wakati siwezi mi kuona? Nikuone mama, niweze tazama Every body say ee-eeh ee-eh ee Ee-eh ee-eh ee, eh Ee-eh ee-eh ee, I love you, nakupenda Tena, ee-eh ee-eh Ee-eh ee-eh ee, eh Ee-eh ee-eh ee, I love you, nakupenda Say ee-eeh ee-eh ee Ee-eh ee-eh ee, eh Ee-eh ee-eh ee, I love you, nakupenda