Daima Kenya

Daima Kenya 歌詞

ジャンルPop
原文言語SW
閲覧数2
歌詞座標

原文歌詞

SW
翻訳はまだありません。原文を表示しています。
18
Umoja ni fahari yetu Undugu ndio nguvu Chuki na ukabila Hatutaki hata kamwe Lazima tuungane, tuijenge nchi yetu Pasiwe hata mmoja Anaetenganisha Naishi, Natumaini Najitolea daima Kenya Hakika ya bendera Ni uthabiti wangu Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani Daima mimi mkenya Mwananchi mzalendo Kwa uchungu na mateso Kwa vilio na uzuni Tulinyakuliwa Uhuru Na mashujaa wa zamani Hawakushtushwa na risasi Au kufungwa gerezani Nia yao ukombozi kuvunja pingu za ukoloni Naishi, Natumaini Najitolea daima Kenya Hakika ya bendera Ni uthabiti wangu Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani Daima mimi mkenya Mwananchi mzalendo Wajibu wetu Ni Kuishi kwa upendo Kutoka ziwa Mpaka pwani Kaskazini na kusini Naishi, Natumaini Najitolea daima Kenya Hakika ya bendera Ni uthabiti wangu Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani Daima mimi mkenya Mwananchi mzalendo