Moyo Mashine

Moyo Mashine 歌詞

ジャンルPop
時間4:19
原文言語SW
閲覧数2.7K
歌詞座標

原文歌詞

SW
翻訳はまだありません。原文を表示しています。
18
Najua kukikucha ntajuta kama nikikuta unanitania Maana moyo wangu nimekupa uweke Mimi ni mfungwa tena ni mjinga Nimejileta gerezani Tena sikuwaza ntakuwa mateka Mmh Najua ulinizungusha sana Sijali huwa ni mambo ya ujana Kukupenda wewe sijuti Maneno yalisemwa mengi sana Kuna wakati nilikata tamaa Kukupenda wewe sichoki (Moyo mashine) Ila majibu ya upendo ulishakosa (Acha waseme) Nimekupendea nini (Moyo mashine) Ila majibu ya upendo ulishakosaga (Wacha waseme) Nimekupendea nini Nafsi inanituma upendo uko nje ya maneno Ila vitendo Kama bubu akipenda atanena vipi kwa maneno Pasina vitendo? Kiziwi, hata ukimwambia nakupenda wata hasikii Ila vitendo oh Wewe sijui sababu za kukupenda Siwezi sema, ila utaona ah Najua ulinizungusha sana Sijali huwa ni mambo ya ujana Kukupenda wewe sijuti Maneno yalisemwa mengi sana Kuna wakati nilikata tamaa Kukupenda wewe sichoki (Moyo mashine) Ila majibu ya upendo ulishakosa (Acha waseme) Nimekupendea nini (Moyo mashine) Ila majibu ya upendo ulishakosaga (Wacha waseme) Nimekupendea nini Oh kama moyo ulisimama nlipokuona Hukuongea, hukucheka, nilikuona tu Na tabia sikufahamu, labda niache mwanadamu Ukipenda usishangae ni upofu wa moyo Kumbe moyo ulinirubuni, hukusema umependa nini (Moyo mashine) Ila majibu ya upendo ulishakosa (Acha waseme) Nimekupendea nini (Moyo mashine) Ila majibu ya upendo ulishakosaga (Wacha waseme) Nimekupendea nini